Share news tips with us here at Hivisasa

Kaunti ya Uasin Gishu in a mipango ya kujenga kituo cha kuifadhi maziwa kwa kima cha shillingi 2.5 milioni.

Kituo hicho kitajengwa katika maeneo ambayo yanaongoza katika uzalishaji wa maziwa mbali na kujengwa kwa vituo vingine katika kila kaunti ndogo.

Waziri wa biashara, viwanda na ushirika katika kaunti hiyo Philip Melly alisema hatua hiyo inalenga kunusuru wakulima kutokana na hasara ambayo wanapata kutokana na kuharibika kwa maziwa wanapoyasafirisha kwa kiwanda cha New KCC mjini Eldoret.

Melly alisema umbali wa kiwanda hicho hufanya wakulima wengi kupata ya hasara mamilioni wakati maziwa yanapoharibika kabla ya kufika katika kiwanda hicho.

Melly aliwataka wakulima kujiunga na vyama vya ushirika ili kupata faida nzuri kutoka kwa mauzo ya maziwa.

''Iwapo wakulima watatumia vyama vya ushirika kuuza maziwa yao watapata faida kubwa ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa kama vile ilivyo kwa wenzao katika kaunti jirani ya Nandi,” aliongeza.

Waziri huyo alisema kwa wakati huu wakulima huuza maziwa yao kwa bei ya rejereja ya shilingi 36 kwa lita moja ambapo alisema iwapo watajiunga na vyama vya ushirika watapata faida bora katika soko la humu nchini.

Akihutubia wakulima Jumanne Melly alisema kutokana na ukosefu wa mpangilio bora wa wakulima kuuza maziwa yao wafanyibiashara wa kati wamekuwa na mazoea ya kuwanyanyasa kwa bei duni.