Muungano wa kutetea maslahi ya waalimu nchini Knut, umepongeza kuhamishwa kwa Jacob Kaimenyi kutoka wizara ya elimu.
Mwenyekiti wa Knut tawi la Nakuru, Njau Kuria amesema kuwa kuhamishwa kwa Kaimenyi kutoka wizara ya elimu kutasaidia kufufua wizara hiyo aliyosema ilikuwa imekufa.
Akiongea jumatano mjini Nakuru,Kuria alisem kuwa Kaimenyi alikuwa mzigo kwa wizara ya elimu na hata sekta ya elimu nchini na kuondoka kwake ni baraka.
"Kwa muda mrefu tumekuwa tukilia kuhusu Kaimenyi na Mungu amesikia maombi yetu na akahamishwa.Sisi kama waalimu tunamshukuru rais Kenyatta kwa kuchukua hatua ya kumhamisha Kaimenyi kwa sababu itaokoa sekta ya elimu," alisema Kuria.
Alimtaka waziri mpya w elimu Fred Matiang'i kutofuata mkondo w Kaimenyi bali ashugulike na kuleta mageuzi yanayohitajika katika sekta ya elimu.
"Kuna mambo mengi sana ambayo yanafaa kutendeka na kutekelezwa katika sekta ya elimu na tunamtaka waziri anayeingia kufanya kila juhudi ya kisafisha wizara hii," alisema.
Aidha aliahidi kuwa Knut iko tayari kushirikiana na waziri Matiang'i katiKa kuleta mageuzi katika sekta ya elimu.
"Waalimu wako tayari kufanya kazi na waziri Matiangi na tutaahirikiana naye katika kuboresha sekta ya elimu ambayo ni muhimu sana katika ukuaji wa taifa letu," aliongeza.