Share news tips with us here at Hivisasa

Kuna matumaini makubwa ya kudidimizwa na kuangamia kwa kundi la kigaidi la Al Shabaab, iwapo vikosi vya kuweka usalama nchini Somali vitafanikiwa kutumia mgawanyiko uliko baina ya makundi hayo.

Haya yamesemwa na waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery siku ya Ijumaa kwenye mkahawa mmoja jijini Mombasa, na kudai kuwa makundi tofauti yamechipuka kutoka kwenye kundi kuu la magaidi hao wa Al Shabab, na huenda makundi hayo yakawa na mizozo ya ndani kwa ndani, hali ambayo italipa jeshi la Amisom nguvu na nafasi mwafaka ya kukabilkiana na magaidi hao.

Ameongeza kusema kuwa ugaidi utashindwa kabisa kwenye eneo hili, na kundi hilo litalegea kwa kukosa wafuasi na wafadhili.

Aidha alitoa furaha yake kuwa hiyo ni furaha kwa nchi za Afrika pamoja na mataifa ulimwenguni ambayo yanapitia changamoto za kiusalama kama zile nchi ya Kenya imepitia kwenye siku za hivi karibuni.

Nchi ya Kenya imekuwa ikilengwa kwa mashambulizi na magaidi ya kigaidi kama Al Shabab na kundi la Al-Qaida, ambapo raia wengi wameangamizwa na mkono dhalimu wa wahalifu hao.

Hata hivyo, alisema kuwa nchi ya Kenya itaendelea kushirikiana na mataifa mengine kupigana dhidi ya makundi hayo ya ugaidi.