Hali ya ati ati imekumba wakaazi wa mtaa wa Rhonda Nakuru kufuatia kukithiri kwa kunguni eneo hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi hao Jumanne walilalamika kwamba hali si hali tena kwani wadudu hao wamekuwa jinamizi kwao.

"Hatupati hata lepe la usingizi kwani kunguni zimetuvamia.Wameenea hadi kwa kuta na kufanya kuwaangamiza kuwa vigumu hata zaidi.Tumejaribu kuzichoma lakini ni kama zinaongezeka tu," alisema Isabel Wambugu, mmoja wa wakaazi hao.

Matamshi hayo yaliungwa mkono na Paul Kimeu aliyeongeza kuwa watoto ndio waliotharika sana.

"Watoto wetu wachanga wameathirika pakubwa kwa kuwa kila wanapovamiwa na hawa wadudu hushinda tu wamelia kwa kukosa kuufuatilia na kuwauwa mwilini," aliongeza.

Aidha wakaazi hao walirai wizara ya afya ya umma kwenye kaunti ya Nakuru kuwaokoa kutkana na kero hilo.