Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wanafunzi wa shule za msingi wanaotarajia kufanya mitihani yao ya kitaifa ya KCPE juma lijalo wameonywa kujiepusha na ushawishi mbaya unaopelekea kushiriki udanganyiifu.

Akiongea katika hafla ya kuwazawadi wanafunzi katika shule ya msingi ya Utange eneo la Shanzu mjini Mombasa siku ya Alhamisi, mwakilishi wa wadi wa Shanzu Maimuna Salim alisema kwamba iwapo wanafunzi watajitenga na watu kama hao, basi visa vya udanganyifu vitapungua.

Kulingana na Maimuna, hatua hiyo imechangia pakubwa kudidimiza viwango vya elimu katika kaunti hiyo, na swala hilo linafaa kuangaziwa vyema kwa kuwashauri wanafunzi kujitenga na watu walio na malengo potovu.

Maimuna, ambaye pia ni kiongozi wa walio wachache katika bunge la kaunti ya Mombasa aliwashinikiza maafisa wa elimu katika kaunti hiyo kuibuka na mbinu mbadala zitakazotumika kuzuia kuchipuka kwa visa vya udanganyifu wa mitihani ya kitaifa.

"Tunawasihi maafisa wa elimu kaunti ya Mombasa kuibuka na mbinu mbadala za kuzuia kuchipuka kwa visa vya udanganyifu wa mitihani ya kitaifa ili wanafunzi wetu waweze kuorodhesha matokeo mazuri," alisema Maimuna.

Kauli ya kiongozi huyo imejiri huku viongozi mbalimbali, maafisa wa wizara ya elimu nchini pamoja na baraza la mitihani wakishikilia kuwa watawakabili barabara wanafunzi watakaopatikana wakishiriki udanganyi