Maafisa wa kusimamia mradi wa maji katikaKaunti ya Nyamira walifika mbele ya kamati ya kuchunguza utumizi wa pesa za serikali ili kueleza jinsi wametumia pesa katika mradi wa maji kwa kaunti hiyo.
Maafisa hao walifika mbele ya kamati hiyo mnamo siku ya Alhamisi katika majengo ya Kaunti ya Nyamira ili kueleza utumizi wa pesa kwa mradi wa maji, na baadaye ilisemekana kuwa maafisa hao walitoa habari ambayo si ya ukweli.
Hii ni baada ya maafisa hao kutoa ripoti yao mbele ya kamati hiyo ripoti ambayo ilikanwa na wamakamati hao na kusema si ya ukweli.
Akizungumza siku ya Alhamisi wakati uchunguzi huo uolikua ukiendelea, mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza utumizi wa pesa za serikali katika Kaunti ya Nyamira Ezra Mochiemo aliagiza maafisa hao kujitayariha kwa wiki moja ijayo ili kueleza jinsi walitumia pesa kwa mradi wa maji baada ya ripoti waliyotoa hiyo jana kutoambatana.
“Jinsi ripoti yenu ilivyo, haina msingi wa utumizi wa pesa za serikali, maana pesa zililipwa wale ambao walikuwa wanafanya kandarasi ya kuweka maji kabla ya kumaliza kazi iyo,” alisema Mochiemo.
“Naomba mjitayarishe ili mje tena kutueleza jinsi mumetumia pesa hizo kwa uwazi,” aliongeza Mochiemo.
Maafisa waliofika mbele ya kamati hiyo ni mkurugenzi wa maji katika Kaunti ya Nyamira Kennedy Bosire na Alloys Machuka .