Mwanaharakati wa haki za vijana katika jimbo la Mombasa Bolton Mwandawiro sasa anataka maafisa wa polisi kufunga mabanda yote yanayoonyesha filamu katika eneo la Changamwe.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Ijumaa, mwanaharaki huyo alidai kuwa wenye maeneo hayo wanatumia biashara yao vibaya na kuwaharibu vijana wachanga kwa kuonyesha filamu za ngono.
''Mabanda mengi ya kutazama filamu hapa Changamwe yanaonyesha video vya ngono, na hii si nzuri kwa vijana wetu kwani wengo wao huathirika kisaikolojia,'' alisema Mwandawiro.
Mwandawiro sasa anataka maafisa wa polisi kuhakikisha kuwa wenye mabanda hao wanatiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka ya kuharibu watoto wa shule.
Aidha, mwanaharakati huyo amewahimiza vijana kutafuta vibarua vidogo vidogo badala ya kujihusisha na tabia zisizowafaidi maishani.