Share news tips with us here at Hivisasa

Maafisa wa polisi wanaosimamia kitengo cha dhuluma za kijinsia wamehimizwa kutumia sheria zilizopo na kuwakabili wanaotekeleza dhuluma hizo.

Akiongea mjini Mombasa siku ya Jumamosi, Afisa mratibu wa mipango wa Shirika la Haki Afrika Francis Auma Gamba alisema kwamba kitengo hicho kina umuhimu mkubwa kwa Jamii.

Alisema kwamba iwapo watawajibikia majukumu yao kikamilifu, basi swala hilo la dhuluma za kijinsia na kingono miongoni mwa jamii zitakomeshwa.

Kulingana na Gamba, Maafisa hao wa usalama wamekuwa wakipokea mafunzo kutoka kwa serikali na mashirika kuhusu jinsi wanavyopaswa kutekeleza majukumu yao katika kukomesha dhuluma wanazotendewa akina mama na watoto.

“Kuna umuhimu wa maafisa wa polisi kujitokeza waziwazi na kuwakabili wabakaji ili kupunguza visa vya ubakaji katika eneo hili na kuiwezesha jamii kuishi kwa amani na kuwakinga watu wao dhidi ya dhuluma hizo," alisema Gamba.

Gamba aliitaka jamii ya Pwani kuchukua muda huu na kuripoti visa vya dhuluma katika vituo ya polisi na afisi za mashirika hayo ili yachukue jukumu la kuwatendea haki waathiriwa.

Hata hivyo harakati zilitengwa na Umoja wa Mataifa ili kukabiliana na dhuluma dhidi ya wanawake na watoto nchini.