Share news tips with us here at Hivisasa

Naibu Gavana wa Kaunti ya Kisii Joash Maangi amehimiza viongozi kuungana ili kuleta maendeleo zaidi katika kaunti hiyo.

Maangi alisema umoja na ushirikiano miongoni wa viongozi utaleta manufaa kwa wakazi.

Akizungumza mjini Kisii siku ya Jumapili, Maangi aliwataka viongozi, wanasiasa na wananchi kushirikiana na serikali ya kaunti ya Kisii ili kuleta maendeleo zaidi.

"Naomba tuungane pamoja na tushirikiane katika miradi mbaimbali kwani umoja utaleta maendeleo miongoni mwetu," alisema Maangi.

Wakati huo huo, Maangi aliomba wahubiri na wakristo wote nchini kuombea viongozi walio mamlakani ili wawe na maarifa ya kuongoza wananchi kupitia maarifa ya Mungu.

Maangi alisema bila Mungu, viongozi hawatakuwa na maarifa ya jinsi ya kuongoza wananchi na kusema kuna haja ya kuwa na maombi ambayo yataleta umoja na heshima miongoni mwa watu wote.

"Bila maombi, viongozi hatutakuwa na maarifa ya kuwaongoza wananchi wa nchi hii. Naomba kila mmoja wetu awe anafanya maombi kwa serikali za kaunti na ile ya kitaifa na kwa viongozi wote," aliongeza Maangi.