Machifu na walimu wameombwa kuwashauri wakazi kujitokeza kujiandikisha kama wapiga kura ili kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao wa 2017.
Akizungumza siku ya Jumapili mjini Nyamira mwenyekiti wa Jomo Kenyatta Foundation Walter Nyambati alisema walimu na machifu wanastahili kutoa ushauri kwa wakazi kujiandikisha kama wapiga kura kwani hao huwafikia wengi wanapofanya shughuli zao za kikazi.
“Naomba walimu na machifu kueleza wakazi umuhimu wa kuwa mpiga kura ili kila moja kuhakikisha anapata kadi ya kura, itakayomwezesha kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo katika taifa la Kenya,” alisema Nyambati.
Wakati huo huo, mwakilishi wa Wadi ya Bigichora Beauttah Omanga aliomba wakazi ambao walijiandikisha kupata vitambulisho kuchukuwa stakabadhi zao na kuvitumia kujiandikisha kama wapiga kura.
“Naomba wale wote waliojiandikisha kupata vitambulisho kuenda kwa kuchukuwa vitambulisho vyao maana kuna vingine ambavyo tayari vimefika, ili kujiandikisha kama wapiga kura,” alisema Nyambati.