Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri ametupilia mbali  shinikizo za  kiongozi wa upinzani Raila Odinga kukashifu serikali kutokana na ziara za rais Uhuru Kenyatta anazofanya nchi za nje, pamoja na sakata inayozunguka fedha za mkopo za EuroBond.

Kimani anasema kuwa madhumuni ya Raila sio kwa nia njema ya Kenya, ila ni kutimiza malengo fulani ya CORD kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017.

Kimani amemsuta Raila akisema anatumia mbinu ya kudanganya wakenya kupitia propaganda, wengi ambao mbunge huyo amesema hawapendi ukweli.

Aidha, Kimani anasema kwamba Raila amealikwa kutoa maelezo kuhusu anachokijua kuhusu Eurobond na waziri wa fedha Henry Rotich pamoja na tume ya kukabiliana na ufisadi nchini EACC, lakini ‘ametoroka’.

“Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (AG) ndiye mwenye jukumu la kuangalia fedha zinavyotumika na kutoa ripoti kama kuna pesa zimepotea. Pesa zote ziliingia kwa Benki Kuu ya Kenya, na AG amesema kwamba anajua akaunti zote pahali ambapo pesa hizo ziliingia,” alisema Kimani akiongea mjini Nakuru Jumanne 8.

Kimani alimchangamoto Raila kutoa ushahidi alio nao kwa mamlaka za kukabiliana na ufisadi nchini.

Mbunge huyo wa kwanza katika bunge la 11, amesema kwamba Raila anatisha tu kwa kusema atatoa taarifa hizo, akihoji tatizo la Rais Kenyatta kwenda nje ya nchi kwa manufaa ya Wakenya.