Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Madereva Mombasa wametakiwa kushirikiana na kutokuwa na chuki kati yao, ili kuleta umoja na undugu miongoni mwao.

Akizungumza na mwanahabari huyu siku ya Jumapili, mmiliki wa matatu kutoka eneo la Bamburi, Salim Hussein, alionyesha kusikitishwa kwake na jinsi baadhi ya madereva walivyokosa maadili na kuchukuwa sheria mikoni mwao pasi kujali maisha ya wengine.

Kauli hii inajiri baada ya dereva wa matatu, katika eneo la Bamburi, kuuwawa kwa kudungwa kisu na mwenzake baada ya kutofautiana kuhusu pesa katika eneo la Bakarani siku ya Jumamosi.

Hussein alikitaja kitendo hicho kama cha unyama na dhuluma na kusisitiza kuwa sheria lazima kuchukuliwa dhidi ya waliotekeleza mauji hayo.

Marehemu, Sule Ali, alidungwa kisu kwa tumbo na mwenzake, baada ya kumzidi nguvu pale alipokuwa anamlazimisha kutoa fedha kulingana na maafikiano yao.

Dereva aliyetekeleza mauaji hayo yuko chini ya ulinzi wa polisi na anasubiri kufunguliwa mashtaka katika mahakama.