Madereva na wamiliki wa Tuktuk kaunti ya Mombasa wameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kutowanyanyasa haki zao za biashara katika maeneo hayo .
Akizungumza na waandishi wa habari katika maandamano ya madereva na wamiliki wa tuktuk Jumatano, mwenyekiti wa chama cha madereva na wamiliki wa tuktuk Obedi Muruli alisema waziri wa usafiri katika kaunti ya Mombasa Tawfiq Balala hapaswi kuamua kufunga barabara ya Digo bila kuwahusisha.
Aidha Obedi alisema kuwa Kaunti ya Mombasa imekuwa ikiwatoza faini za juu kwa kuitumia barabara hiyo bila ya kuwajulisha rasmi kufungwa kwa barabara ya Digo .
Kwa mujibu wa madereva na wamiliki wa tuktuk waliishtumu hatua ya maafisa wa usalama wa kaunti ya Mombasa kuwapiga ili kusitisha mandamo yao.