Share news tips with us here at Hivisasa

Madereva na wamiliki wa Tuktuk kaunti ya Mombasa wameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kutowanyanyasa  haki zao za biashara katika maeneo hayo .

Akizungumza na waandishi wa habari  katika  maandamano  ya madereva na wamiliki wa tuktuk  Jumatano, mwenyekiti wa chama cha madereva na wamiliki wa tuktuk Obedi Muruli alisema  waziri wa usafiri katika kaunti ya  Mombasa  Tawfiq Balala hapaswi kuamua kufunga barabara ya Digo bila kuwahusisha.

Aidha Obedi alisema kuwa Kaunti ya Mombasa imekuwa ikiwatoza faini za juu kwa kuitumia barabara  hiyo bila ya kuwajulisha rasmi kufungwa kwa barabara ya Digo .

Kwa mujibu wa madereva na wamiliki wa tuktuk waliishtumu hatua ya maafisa wa usalama  wa kaunti ya Mombasa kuwapiga ili kusitisha mandamo yao.