Wanachama watano wa vuguvugu la MRC wanaokabiliwa na mauwaji ya polisi wanne watasalia rumande hadi siku ya Alhamisi, kusubiri mahakama kuu kutoa uamuzi iwapo wana kesi ya kujibu au la.
Mnamo machi 3, 2013 katika eneo la Miritin huko Jomvu, washukiwa Jabair Ali Dzuya, Bwana Mkuu Jabu, Antony Mwatela, Badi Saidi Kassim na Omari Salim Juma wanadaiwa kuwashambulia kwa mapanga na risasi maafisa wa polisi Salim Limutai Chebi, Stephen Maithiya,Andrew Sugwa na Otieno Owour.
Mwendesha mashtaka Jamii Yami alimtaka jaji Martin Muya siku ya Jumatatu kuzingatia ushahidi uliotolewa na mashahidi wa kesi hiyo ili haki itendeke kwa familia za maafisa waliofariki.
Kesi hiyo sasa inatarajiwa kuskizwa Alhamisi hii.