Mahakama kuu ya Mombasa imemuachilia huru mwanamume anayedaiwa kuhusika na kosa la mauwaji.
Mnamo Februari 13, 2013 katika eneo la Kisauni, mshtakiwa anadaiwa kumuuwa Issa Hamisi.
Jaji katika mahakama kuu ya Mombasa Martin Muya, alisema siku ya Ijumaa kuwa kulingana na ushahidi uliotolewa hauambatani na kumuhusisha mshukiwa huyo na mauwaji hayo.
Mshukiwa alisalia rumande tangu kushikwa kwake tangu mwaka 2013.