Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama ya mji wa Kisii imepongezwa kwa kuonyesha haki na uwazi kwa wakazi wa kaunti hiyo.

Hii ni baada ya mahakama hiyo kumuhukumu mwanamume mmoja kwa jina Lucas Misati adhabu ya kifungo cha miaka mia mbili gerezani kwa kosa la kuwaua watoto wake wanne mwaka wa 2012.

Jaji wa mahakama hiyo Joseph karanja alifanya uhamuzi huo baada ya kubainika kuwa mwanamume huyu aliwaua watoto wake wanne kwa kuwadunga kisu huku mkewe akifanikiwa na kutoroka. 

Akizungumza siku ya Jumatano katika eneo la Bobarancho mjini Kisii mamake mfungwa huyo Alexina Nyanchama alipongeza mahakama kwa kutendea haki wakaazi kwani mwanawe alikuwa amefanya visa vingi vya kutamausha katika kijiji hicho.  

“Mahakama ya kisii imeonekana kufanya kazi yake kwa njia ya uwazi maana haki imetendeka .Tunaomba mahakama zote nchini kuwa na mfano wa aina hiyo,” alisema Nyanchama.