Share news tips with us here at Hivisasa

Takriban makurutu 108 walijeruhiwa Jumapili kufuatia mkanyagano baada ya transfoma kulipuka katika chuo cha mafunzo ya huduma za vijana kwa taifa NYS huko Gilgil. 

Majeruhi wa mkasa huo walikimbizwa na shirika la msalaba mwekundu katika hospitali ya kaunti dogo ya Gilgil.

Afisa mkuu wa hospitali hiyo Dr Catherine Gitau anasema kuwa baadhi ya majeruhi walihamishiwa hospitali ya level 5 Nakuru kwa matibabu zaidi.

Naye afisa msimamizi wa hospitali hiyo ya Nakuru level 5 John Murima amethibitisha kwamba makurutu sita wa NYS wanapokea matibabu katika hospitali hiyo. 

Ameongeza kuwa watano miongoni mwao ni wa kike.