Share news tips with us here at Hivisasa

Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago amesema kuwa ataendelea kujihusisha na maswala ya kaunti ya Nandi akisema kuwa ni haki yake.

Akihutubia wanahabari nje ya vikao ya bunge la Uasin Gishu baada ya kufungua rasmi vikao vya bunge hiyo siku ya Jumanne, Mandago amefutitila mbali onyo lililotolewa kwake kukimya kuzungumzia maswala na maendeleo ya kaunti ya Nandi na badala yake kujihusishwa na kaunti ya Uasin Gishu.

"Ninawaambia wapinzani wangu, mimi ni Mnandi na hili linanipa huru ya kuzungumzia maswala ya Nandi, nitaendelea kuzuru kaunti hiyo, sina hatia,” alisema Mandago.

Haya yanajiri baada ya mkaazi wa Nandi Kiprotich Cherargei wiki iliyopita kumyoshea kidole cha lawama Mandago kuwa anazipa kipao mbele maswala ya kaunti ya Nandi badala ya kuzihusisha na maswala ya kaunti ya Uasin Gishu, kaunti ambayo aliteuliwa kuiongoza.