Share news tips with us here at Hivisasa

Wazazi katika wilaya ya Marani, kaunti ya Kisii wametishia kuelekea mahakamani kuzishtaki shule ambazo zitaongeza karo zao kinyume na agizo la serikali ya kitaifa.

Hii ni baada ya naibu rais William Ruto kusema kuwa serikali kuu hulipia wanafunzi wa shule za umma kiwango fulani cha pesa kwa kila mwanafunzi wa sekondari huku akiongezea kwamba walimu wakuu sharti wafuate maagizo ya wizara ya elimu.

Wakizungumza na waandishi wa habari jumatatu mjini Marani, wazazi hao wakiongozwa na mwenyekiti Peter Ongoro, walisema kuwa baadhi ya shule za upili zimeongeza karo kupita kiasi na kutishia kuelekea mahakamani kuzishtaki shule husika.

Pia, walisema mwaka huu, karo za shule zimeongezwa kwa asilimia kubwa kando na matamshi ya Ruto aliyewaonya walimu wakuu kutoongeze karo .

“Shule nyingi za upili katika wilaya ya Marani zimeongeza pesa katika mwaka huu hasua muhula wa kwanza. Tunapoulizia ni kwa nini  wanasema ni mwazo wa mwaka na kuahidi mihula mingine kupunguza. Sisi hatutakubali maana naibu wa rais alisema tukiongezewa karo kwa kiwango kile kimewekwa turipoti kwa kamishena wa kaunti,” alisema Peter Ongoro.

“Sisi tumeamua tutawashtaki walimu wakuu wa shule hizo dhidi ya nyongeza ya karo kwa shule kupita kiasi ,” aliongeza Ongoro.

Ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha mtoto wake amepata masomo na kulalamikia ongezeko la karo kiholela.