Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya umeme nchini Kenneth Marende ameipongeza hatua ya serikali ya kuanzisha mradi wa 'Mwangaza Mitaani', uliozinduliwa siku ya Ijumaa mjini Mombasa.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa watajitahidi kama kampuni kwa ushirikiano na serikali kuhakikisha Wakenya wote wanapata umeme kwa gharama ya chini.

Akiongea mjini Mombasa siku ya Ijumaa wakati wa uzinduzi huo, spika huyo wa zamani alisema kuwa mipango hiyo itakamilika ifikiapo mwaka ujao.

“Sisi tumejipanga na tutahakikisha angalau asilimia sabini ya Wakenya wanapata umeme kufikia mwaka ujao,” alisema Marende.

Kwa upande wake, waziri wa kawi nchini Charles Keter alisema kuwa mpango huo wa umeme ni hatua muhimu hasa kwa vijana kuendesha na kupanua biashara zao.

Vile vile aliitaja sekta ya utalii katika ukanda wa Pwani kama sekta itakayoimarika pakubwa, kwa kusema shughuli nyingi zitaweza kufanyika hata wakati wa usiku bila hofu yoyote.