Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Waziri wa elimu Fred Matiang’i ameombwa kuingilia kati masuala ya walimu ili mahitaji yaafikiwe kikamilifu.

Mwenyekiti wa Wakfu wa Jomo Kenyatta (JKF), Walter Nyambati aliomba Waziri Matang’i kujaribu kila awezalo kujadili na chama cha walimu nchini Teachers Service Commission (TSC ) jinsi mahitaji ya walimu yatashughulikiwa na kuafikiwa kikamilifu huku nyongeza yao ya mishahara ikiwa mojawapo.

Kulingana na Nyambati walimu wanastahili kutendewa haki yao ili kuendelea kufanya kazi yao kwa moyo mmoja badala ya kutarajia wasiloliona kwa muda mrefu.

“Walimu wanastahili kushughulikiwa na ninaomba waziri Matiang’i kuangilia kati ili mahitaji yao yashughulikiwe,” alisema Nyambati.

Wakati huo huo, Nyambati alisema baadhi ya shule zipo na uhaba wa walimu wa kutosha na kuomba Matiang’i kusuluhisha changamoto hiyo kwa kuongezea walimu katika shule hizo.

Aidha, aliomba wanafunzi wa shule zote za kaunti kutia bidii katika masomo ili kujiendeleza na kutengeneza maisha yao katika siku za usoni.