Mwakilishi wa wanawake katika Kaunti ya Mombasa Mishi Mboko ametoa tahadhari kwa wapiga kura katika eneo bunge la Malindi, kuwa kwa kupigia kura upande wa serikali wa JAP, wawe tayari kudhulumiwa zaidi na serikali hiyo ambayo alidai bado haijaonekana kushughulikia masuala yao kwa njia sawa.
Akiongea siku ya Jumatano kwenye harakati za kumalizia kampeni ya kiti cha eneo bunge la Malindi, Mboko alisema kuwa wananchi wasikubali kuchezewa shere na chama cha JAP ambacho kinatumia nafasi hii kuwashawishi wakazi ilhali bado wakazi wa eneo hilo la Pwani kwa jumla wana mengi ambayo hawajatimiziwa.
Itakumbukwa kuwa viongozi wa kisiasa kutoka upande wa serikali na wa upinzani wamepiga kambi katika eneo bunge hilo tangu wiki jana kujaribu kuwashawishi wapiga kura kutoka eneo bunge hilo la Malindi kuwapigia wawaniaji wa vyama husika kura, huku wakionekana kuwaahidi mambo kadhaa iwapo wakazi watapiga kura kwenye vyama vyao.
Kiongozi wa muungano wa upinzani wa Cord Raila Odinga hakusita kuendeleza shtuma zake dhidi ya serikali ya Jubilee kwa kile alichotaja kama kukithiri kwa ufisadi serikalini.
Aidha, alikosoa serikali kwa kutowaelezea Wakenya kuhusiana na masuala mengi ambayo upande wa upinzani imezua hivi majuzi kuhusiana na ufisadi.
Odinga aliwataka wakaazi wa Pwani kwa jumla kuendelea kuunga mkono muungano wa Cord na kupiga kura kwa wengi kwa mgombeaji wa ODM Willy Mtengo