Share news tips with us here at Hivisasa

Kiongozi wa wanawake katika kaunti ya Mombasa Mishi Mboko anamtaka seneta wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko kuwaomba msamaha wakazi wa Mombasa kwa kile amekitakata kama kuwakosea heshima viongozi wao.

Mboko ameyataja matamshi aliyatoa Mike Sonko siku ya Jumamosi katika hafla ya kuwapa hati miliki wakazi wa shamba lenye utati la Waitiki, kuwa ya kumdhalilisha Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hasaan Joho.

Akizungumza nyumbani kwake siku ya Jumapili alipoandaa maandamano yaliyowaleta pamoja zaidi ya wanawake 500, Mboko alimtaja seneta Sonko kama kiongozi asiye na heshima na nidhamu kwa viongozi wenzake.

"Ikiwa kwao alifundishwa matusi sisi hapa Mombasa tunawapa heshima wadogo kwa wakubwa, hatujui kuyatamka matusi vinywa vyetu,"  alisema Mboko.

Mboko vilevile alitika serikali litafakari upya malipo ya shamba la Waitiki huku akiwataja wakazi wanaoishi katika shamba hilo kama wananchi wasiojiweza kiuchumi.

Siku ya Jumamosi, seneta wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko aliwataja viongozi wa upinzani kuwa wasaliti wakuu wa serikali na kuwa hawana heshima kwa Rais.