Share news tips with us here at Hivisasa

Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua amesema kuwa serikali yake itaipa kipaumbele sekta ya elimu na kuhakikisha kwamba kila mtoto katika kaunti ya Nakuru anajiendeleza kimasomo pasi ubaguzi wowote.

Akizungumza Jumanne mjini Nakuru wakati wa kuwasilisha hundi ya shilingi milioni 55 za ufadhili wa elimu kwa watoto wasiyojiweza, gavana huyo alisema sekta ya elimu iko wazi kwamba kila mtoto sharti apate elimu.

"Sisi kama serikali ya kaunti ya Nakuru tutalipa kipaumbele swala la elimu na tutahakikisha kwamba kuna ufadhili wa kutosha ili tuimarishe kaunti yetu kupitia elimu,'' Mbugua alisema.

Wakati huo huo, ametoa wito kwa wazazi kukumbatia swala la elimu kwa mtoto pasi ubaguzi akisema elimu ni nguzo muhimu kwa familia, kaunti na hata taifa.

"Nawaomba wazazi mchukulie kwa uzito swala la elimu kwa watoto manake hakuna kitu bora kama kuelimisha mtoto ili afanikiwe maishani,"Mbugua alisema.

Naibu gavana Joseph Ruto aliunga mkono msimamo huo.

"Sisi tunajua Kaunti ya Nakuru inaendelea kupaa manake hata mwaka jana KCPE tuling'ara sana kwa kutoa mwanafunzi wa kwanza,"Ruto alisema.