Gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua amehimiza umuhimu wa kila mtoto kupata elimu katika kaunti ya Nakuru.
Akizungumza Jumanne katika wadi ya Elburgon wakati wa kupeana sare za shule kwa wanafunzi kutoka jamii maskini, Mbugua alisema kuwa elimu ni nguzo muhimu ya maendeleo.
"Ni vyema tufahamu umuhimu wa elimu kwa mtoto na ni elimu tu ambayo itaimarisha maendeleo," Mbugua alisema.
Ameongeza kuwa serikali yake itazidi kushirikiana na serikali kuu katika kuhakikisha kwamba kila mtoto anapata elimu.