Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa eneo bunge la Jomvu Badi Twalib ameunga mkono pendekezo la Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan Joho kuwa kiasi cha fedha za CDF ziekweze katika miradi ya vijana kama vile ujenzi wa vyuo vya viufundi.

Akiongea na mwanahabari huyu katika afisi yake siku ya Jumatatu, mbunge huyo alisema kuwa hilo ni jambo la kufurahisha na kumpa moyo kwasababu kuna baadhi ya vijana ambao wamekaa majumbani tu.

Aliongeza kuwa atahakikisha kuwa vyuo hivyo havitakuwa vya gharama ya juu kwasababu baadhi ya wakaazi wa eneo la Jomvu hawana kipato kizuri.

Wakati huo huo, pia alisema kuwa mradi huo hautakuwa na athari yoyote kwa fedha za CDF kwasababu ni miongoni mwa miradi ambayo inastahili kufanyika katika maeneo bunge.

Badi alisema kuwa vyuo hivyo vitapunguza gharama ya usafiri kwasababu wanafunzi ambao wamekuwa wakisafiri nje ya bunge lake hawatasumbuka tena.

Mbunge huyo alisema kuwa hapo awali, alikua amenzisha mradi sawia na huo katika eneo bunge lake na zaidi ya vijana 250 wamenufaika kutokana na mradi huo, huku akiwaomba wabunge wenzake kushirikiana na kusaidi katika kuwasaidia vijana mitaani.

Gavana Joho amewataka wabunge wote katika Kaunti ya Mombasa kutenga kiasi fulani cha pesa ambacho kitasaidia vijana.