Share news tips with us here at Hivisasa

Walimu na wanafunzi wa shule ya msingi na ile ya upili ya Riakworo wana sababu ya kutabasamu baada ya mbunge wa Kitutu Masaba Timothy Bosire kuipokeza shule hiyo hundi ya shillingi millioni moja siku ya Jumatano.

Pesa hizo zinatarajiwa kusaidia kukarabati shule hizo. 

Akihutubu kwenye hafla hiyo, Bosire alisema kuwa afisi yake iko tayari kuhakikisha kuwa inafadhili shule za eneo hilo kwa vitabu na vifaa muhimu ili kuimarisha masomo, huku akiwahimiza wazazi na kushirikiana ili kuhakikisha kuwa viwango vya elimu vinaimarika katika eneo hilo. 

"Afisi yangu uko tayari kuhakikisha kuwa tunafadhili shule na vitabu na hata pia kuhakikisha kuwa ukarabati wa shule unafanywa na sasa lililobaki ni kwa walimu na wazazi kushirikiana kuhakikisha kuwa viwango vya elimu vinaimarika katika eneo hili," alisema Bosire. 

Aidha aliongeza kusema kuwa ataweka mikakati ya kuhakikisha kuwa viongozi wa kisiasa hawaingishi siasa kwenye usimamizi na uongozi wa shule, huku akisema kuwa siasa hurudisha nyumba viwango vya elimu katika shule nyingi. 

"Mimi sipendi kuingisha siasa kwenye uongozi na usimamizi wa shule zetu. na ni onyo langu kwa wanasiasa wengine wenye mazoea ya kuingisha siasa kwenye masuala ya shule na wacha wajue kuwa kamwe sitaruhusu hali hiyo kwa kuwa siasa za aina hiyo huathiri pakubwa viwango vya elimu katika shule zetu," aliongezea Bosire.