Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Seme James Nyikal amekemea namna ufisadi ilivyokita mizizi katika serikali ya Jubilee, huku mlipa ushuru akizidi kuubeba mzingo wa kupanda kwa gharama ya maisha.

Nyikal ameelezea kughadhabishwa kwake na jinsi baadhi ya viongozi wa kisiasa wametajwa kushiriki katika kashfa hiyo, ilhali wamekuwa katika mstari wa mbele kuwadanganya wananchi.

Mbunge huyo alisisitiza kuwa ingekuwa vyema iwapo pesa zilizopotea za shirika la huduma kwa vijana NYS zingetumika vyema kwa manufaa ya mwananchi wa kawaida.

Aidha, amemtaka kiongozi wa taifa Uhuru Kenyatta kulivalia njuga swala hilo na kutishia kuwa huenda wakaandaa mswada bungeni wa kutokuwa na imani na rais iwapo hatachukua tahadhari za mapema.

“Ufisadi nchini unaendelea kuongezeka kila uchao bila hatua madhubuti kuchukuliwa. Kwa sasa kinachoshubiriwa kwa hamu ni hatua itakayochukuliwa na Rais Kenyatta kudhibiti ufisadi hasaa ikizingatiwa viongozi waliohusishwa na sakata ya NYS ni viongozi wakuu serikalini,” alisema Nyikal.