Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwakilishi wadi ya Flamingo Nakuru Moses Gichangi amekanusha madai ya kusafirisha wapiga kura kutoka wadi nyingine hadi kwake. Katika mahojiano nje ya majengo ya bunge la kaunti ya Nakuru, Gichangi alisema kuwa madai hayo ni njama tu ya wapinzani wake kumchafulia jina.

"Sijawai safirisha wapiga kura, ni njama tu ya wapinzani wangu kuniharibia sifa"Gichangi alisema.

Wakati huo huo aliwataka wakaazi kuzingatia sera za wanasiasa kabla ya kuwapigia kura.

Alisema kuwa kiongozi mwenye maono ya maendeleo ndiye atakayefaa hata katika karne hii.