Mwakilishi wadi ya Elburgon Florence Wambui amewashtumu wale wanaopiga vita uongozi wa gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua. Akizungumza Jumamosi katika hafla moja mjini Nakuru, MCA Wambui amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaopinga juhudi za maendeleo.
"Gavana Mbugua anafaa kuachwa atekeleze wajibu wake wa maendeleo kwa mwananchi" Wambui alisema.
Wakati huo huo amesema kuwa wanawake wa kaunti ya Nakuru watazidi kupigania haki zao kando na pingamizi.
Alisema kuwa wanawake hawafai kudhulumiwa kwa vyovyote katika jamii.
"Katiba iko wazi kuhusu haki za wanawake na hatutakubali kuona wanawake wakidhulumiwa," MCA Wambui alisema.