Hatua ya taifa la Kenya kukabiliana na changamoto zinazoikumba sekta ya utalii zimefanikiwa baada ya mataifa ya magharibi kushirikiana na taifa la Kenya na kuwaruhusu raia wao kuzuru Kenya na hasa mji wa Mombasa.
Kupitia juhudi hizo, zaidi ya watalii elfu moja kutoka mjini Mahia kisiwa cha Ushelisheli wamewasili Bandarini Mombasa ili kuimarisha sekta ya utalii iliyokumbwa na changamoto kutokana na mataifa ya magharibu kuondoa marufuku ya raia wao kutozuru nchini Kenya.
Akiongea na wanahabari mjini Mombasa siku ya Ijumaa baada ya kupokea watalii hao, Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya utalii nchini Muriithi Ndegwa alisema watalii hao wataelekea kisiwa cha Zanzibar nchini Tanzania baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kutalii katika mbuga za wanyama Pwani.
Ndegwa alisema watalii hao kutoka mataifa ya Marekeni, Uingereza, Ushelisheli, na mataifa mengine wameingia Pwani ya Kenya kwa Meli ya Mv Nautica baada ya serikali kuu kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta hiyo na idara ya usalama na kuimarisha usalama Pwani ya Kenya.
"Tumeshukuru serikali kuu kwa ushirikiano na mataifa ya magharibi kuimarisha usalama na kuwawezesha watalii kuzuru humu nchini, hatua hii itasaidia kuimarisha utalii hapa nchini baada ya kusambaratika kwa kiasi kubwa kutokana na mataifa ya magharibi kupiga marufuku raia wao kuzuru humu nchini," alisema Ndegwa.
Wakati uo huo amesema kwamba juhudi za wanajeshi wa majini wa Kenya kwa ushirikiano na mataifa ya magharibi kumesambaratisha kukithiri kwa maharamia katika bahari hindi ambayo wamekuwa wakiteka nyara meli katika maji makukuu na akasema kwamba kuimarisha kwa usalama wa majini kumesaidia pakubwa sekta hiyo.
Hatau ya kuwasili wa watalii hao humu nchini kunatarajiwa kuimarisha sekta hiyo ili kumbwa na changamoto nyingi baada ya kushughudiwa kwa misukosuko wa kiusalama humu nchini.