Meneja wa kampuni ya sukari ya Ramisi iliyoko kaunti ya Kwale amefikishwa mahakamani Mombasa kwa madai ya kuajiri raia kutoka India bila vibali vya kufanya kazi humu nchini.
Mahakama ilielezwa kuwa kati ya Septemba 24, 2015 na Oktoba 27, 2015 , Patrick Chebosi anadaiwa kumuajiri kinyume cha sheria Mahetre Bopu Dattatrya, ambaye ni raia wa India kufanya kazi ya ufundi katika kampuni hiyo.
Wakati huo huo, meneja huyo amekabiliwa na shitaka jingine la kukataa kuwakabidhi maafisa kutoka afisi ya uhamiaji vyeti vya kusafiria na kuzaliwa wafanyikazi wengine wa nchi ya Idia.
Chebosi alikanusha mashitaka yote mbele ya hakimu wa Mombasa Diana Mwachache.
Meneja huyo atasalia kizuizini hadi siku ya Ijumaa ili kusubiri uamuzi wa kupewa dhamana.