Miili miwili na iliyokuwa imesalia katika bwawa la Masinga baada ya ajali ya Mashua halo siku ya Alhamisi wiki hii imepatikana.
Kulingana na chifu wa kata ya Muthesya Benjamin Musyoka miili hiyo miwili ilonekana ikielea katika bwawa hili na mvuvi mmoja aliyekuwa akivua samaki.
Mvuvi huyo aliyekuwa akivua samaki leo, Februari 27, 2016 mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi aliitisha usaidizi kutoka kwa wavuvi wenzake ili kuizoa miili hiyo kutoka majini.
Aidha Chifu huyo alisema kuwa inaaminiwa hakuna miili mingine imesalia katika bwawa hilo na iwapo ipo itapatikana.
"Kwa sasa miili iliyopatikana ni mitano na tuna imani kuwa hakuna mingine iliyosalia," alisema Musyoka.
Kwa sasa miili iliyopatikana katika bwawa hilo tangu siku ya ajali imefikia tano.
Vongozi kadhaa kutoka kaunti ya Machakos akiwepo naibu wa gavana wa kaunti ya Machakos Bernard Kiala na mwakilishi wa wanawake wa kaunti hio Susan Musyoka walifika katika eneo hilo halo Siku ya Ijumaa na kupatiana rambirambi zao na kuzifariji familia za waliofiwa.