Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamke mmoja mnamo Jumatano aliwasilisha kesi kwenye mahakama ya watoto jijini Kisumu, akimshtaki mumewe kwa madai ya kukataa kumlipia mtoto wao karo ya shule ya upili.

Alice Anyango alimshtaki mumewe Tom Omollo, kwa kudinda kulipa karo ya mtoto huyo.

Hata hivyo, mshtakiwa lijitetea akisema kuwa anataka binti yake arejelee darasa la nane ili apate alama zitakazomuwezesha kujiunga na shule ya upili ya kitaifa.

Msichana huyo alipata alama 324 kwenye mtihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) wa mwaka jana. 

Hakimu mkaazi wa mahakama ya watoto jijini Kisumu Angeline Adao, aliwaagiza wazazi hao kutafuta pesa za kumlipia mtoto huyo karo ya shule ya upili, na kuziwasilisha kortini Februari 3.