Mke wa gavana wa kaunti ya Nyamira Naomi Nyagarama amewahimiza kina mama katika kaunti ya Nyamira kuwekeza pakubwa kwenye masomo ya mtoto msichana. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubu kwenye hafla ya kusherehekea siku ya kina mama ulimwenguni katika Parokia ya kanisa Katholiki ya Nyamira, Nyagarama alisema kuwa kwa muda sasa elimu ya mtoto msichana imekuwa ikidhalilishwa, hali ambayo inachangia katika kurudisha nyuma taifa hili kimaendeleo. 

"Elimu ya mtoto msichana ni muhimu sana kwa ukuaji wa taifa hili na sharti sisi kina mama tuwe katika mstari wa mbele kuhakikisha kwamba tunawaelimisha wasichana," alisema Nyagarama.

Aidha aliwahimiza kina mama kujiunga kwenye makundi ili kuchukua mikopo ya kujistawisha kimaisha kutoka kwa mashirika ya kifedha. 

"Ni ombi langu kwenu kina mama kuhakikisha kuwa mnajiunga kwenye makundi ili kuchukua mikopo kutoka kwa mashirika ya kifedha ili kujistawisha," aliongezea Nyagarama.

Picha: Mke wa gavana Nyagarama Naomi Nyagarama. Amewahimiza wakazi kuwapa watoto wasichana kipa umbele katika maswala ya elimu.  WMaina/Hivisasa