Mke wa gavana wa kaunti ya Nyamira Naomi Nyagarama amewataka wazazi na walezi katika kaunti hiyo kutowalazimisha wanao kurudia kidato cha nne kwa sababu ya kufeli mitihani. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubia wakazi wa kaunti ya Nyamira kwenye parokia ya kanisa Katholiki ya Nyamira, Nyagarama alisema kuwa haifai wazazi kuwalazimisha wanao kurudia masomo ya kidato cha nne kwani hali hiyo huathiri pakubwa matokeo ya mitihani. 

 "Ningependa kuwaomba wazazi kutowalazimisha wanao kurudia masomo ya kidato cha nne baada yao kukosa kuafikia alama fulani kwa maana hali hiyo huenda ikaathiri alama anazoweza kuzoa mwanafunzi," alisema Bi Nyagarama.

Nyagarama aidha aliongeza kwa kuwahimiza wazazi kuwaruhusu wanao kujiunga na vyuo vya kiufundi ili kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi utakao wafaa maishani. 

 "Watu wengi hufikiria kwamba mtu anaweza tu akafanikiwa maishani kwa kupata masomo ya chuo kikuu, ila wanalokosa kujua ni kwamba watu wengi wamejiendelesha kwa kutegemea kazi za kiufundi, na ndio maana nawahimiza wazazi kuwaruhusu wanao kujiunga na vyuo vya kiufundi," aliongezea Nyagarama.

Picha. Mke wa gavana wa kaunti ya Nyamira Naomi Nyagarama. Amewataka wazazi na walezi katika kaunti hiyo kutowalazimisha wanao kurudia kidato cha nne kwa sababu ya kufeli mitihani. Maktaba