Share news tips with us here at Hivisasa

Wakulima wa majani chai katika kituo cha ununuzi cha Nyasiongo wamempongeza mbunge wa eneo bunge la Borabu Ben Momanyi dhidi ya kuwakabidhi hundi ya shillingi 100,000 ili kutengenezea paa la kituo hicho.

Haya yanajili baada ya mbunge huyo kuwapa pesa hizo ili kutumika kutengenezea paa hilo na kuweka mabati ili kutonyeshewa.

Wakizungumza na mwandishi huyu wa habari siku ya Alhamisi katika kituo hicho cha Nyasiongo, wakulima hao wakiongozwa na George Misati walisema Momanyi amewasaidia pakubwa kwa kuwapa pesa hizo.

Wakati huo huo, wakulima hao waliomba mbunge wao kupeleka mswada katika bunge la kitaifa kujadili jinsi soko mpya ya majani chai itatafutwa katika nchi za ng’ambo ili kuwanufaisha kujiendeleza kupitia kilimo hicho.

Kulingana na wakulima hao, pesa ambazo hupewa kwa kila kilo hazitoshi kuwanufaisha, na kuomba kutafutiwa soko kimaitafa ambapo majani chai yao yatauzwa.

“Pesa zile tunapewa kwa kila kilo ni kidogo zaidi, tunaomba mbunge wetu kupeleka mswada bungeni ili kujadiliwa na serikali itutafutie soko nzuri ili nasi tuweze kufaidika na kujiendeleza kupitia mumea wa majani chai,” alisema Misati.