Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hali ya taharuki imetanda katika eneo bunge la Malindi baada ya ripoti za kijasusi kudai kuwa kundi lililoharamishwa la The Mombasa Republican Council almaarufu MRC linapanga njama ya kutekeleza mashambulizi na kuvurugu uchaguzi mdogo wa Malindi.

Hii ni baada ya maafisa wakuu wa polisi kutoka kaunti ya Mombasa, Kilifi, Tana River na Kwale Pwani ya Kenya kudai kupokea ripoti hizo za kijasusi kutoka kwa maafisa wa upelelezi.

Kamishna wa Mombasa Nelson Marwa alisema kuwa ripoti hizo zinaonyesha wazi kuwa baadhi ya wanasiasa kutoka Pwani ya Kenya wanafadhili kundi hilo la vijana ili kuzua vurugu na kutatiza uchaguzi huo mdogo.

"Tumepokea ripoti hiyo na maafisa wa polisi wametumwa kushika doria na kubakiliana na kundi lolote la kihalifu litakalojitokeza kuvua vurugu kuharibu uchaguzi huo," alisema Marwa.

Uchaguzi huo mdogo wa Malindi ambao mchakato wa kisiasa kwa sasa umeonekana kupamba moto huenda wapiga kura wakasusia  iwapo usalama utakosa kuimarisha jinsi wanavyotarajia.