Share news tips with us here at Hivisasa

Msanii wa nyimbo za injili Daniel Njogu ametoa wito wa amani miongoni kati ya wananchi. 

Katika mahojiano ya moja kwa moja na mwanahabari huyu, Njogu, ambaye amezindua rasmi kanda mbili za kuhimiza amani katika jamii amesema kuwa pasina amani, taifa hili haliwezi kusonga mbele.

"Ningependa kuwahimiza wananchi tudumishe amani manake ndio nguzo muhimu katika maendeleo ya taifa," alisema Njogu.

Wakati huo huo, ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuhakikisha kwamba wanawaunganisha wananchi, na kusisitiza kuwa siasa hazifai kutumika kuwagawanisha wakenya. 

Ameyasema hayo wakati wa mahojiano katika dhehebu la PCEA Bethsaida Nakuru siku ya Jumapili.