Mahakama moja ya Nakuru ilimwachilia mshukiwa wa mauwaji kwa dhamana ya Sh 350, 000 na mdhamini wa kiasi sawa siku ya Jumatatu.
Ni uamuzi uliotolewa na jaji wa mahakama ya Nakuru Maureen Odero baada ya mashahidi kukosa kufika mahakamani kutoa ushahidi.
Aidha, ni hatua iliyomfanya jaji Odero pia kuahirisha kesi hiyo hadi mwezi Februari.
Mshukiwa Wesley Kipng’etich anadaiwa kumuua Paul Kipkemoi mwezi Machi mwaka wa 2014 katika kaunti ya Narok.
Wakili wa mshtakiwa aliarifu mahakama kwamba mteja wake hajatimiza umri wa miaka 18 akitaka mahakama kutilia maanani hilo inapotoa uamuzi wake na pia kuharakisha kusikizwa kwa kesi hiyo.
Aidha, jaji huyo aliamuru uchunguzi huo ufanywe ili kubainisha iwapo mshtakiwa huyo ana matatizo ya kiakili au la ili aweze kuruhusiwa kujibu shtaka hilo.