Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamme mmoja mwenye umri wa makamo anayedaiwa kumbaka mtoto alifikishwa kwenye mahakama ya Nakuru Ijumaa.

Mshtakiwa huyo anayefahamika kama Nicholas Tanui anadaiwa kumtendea unyama huo mtoto mwenye umri wa miaka kumi na sita Januari 15 mwaka huu katika mtaa wa London ulio viungani mwa mji wa Nakuru.

Kulingana na upande wa mashtaka, mshtakiwa huyo alimwacha mtoto huyo na majeraha baada ya kumtendea unyama huo.

Licha ya hayo, mshtakiwa huyo alikanusha shtaka hilo mbele ya hakimu mkuu wa Nakuru Maroro Nyakundi .

Kesi hiyo sasa itasikizwa Machi 16.