Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamme anayedaiwa kumbaka na kumuua mtoto wa miaka 13 atafunguliwa mashtaka ya mauwaji katika mahakama kuu ya Mombasa.

Hii ni baada ya mwendesha mashataka kutoka afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Erick Masila kuithibitishia mahakama ya chini ya Mombsa siku ya Alhamisi kuwa kutokana na uchunguzi uliofanywa, mshukiwa huyo alihusika katika mauwaji hayo.

Aidha, Masila ameongeza kuwa mshtakiwa anafaa kufunguliwa mashtaka ya mauwaji katika mahakama kuu.

Wiki iliyopita, hakimu Diana Mochache aliagiza Manfred Otieno kusalia rumande ili kufanyiwa uchunguzi wa akili, kupewa matibabu ya majeraha ya mkono na kusubiri uchunguzi wa upasuaji kufanyiwa mtoto aliyebakwa.

Otieno alifikishwa mahakamani wiki iliyopita kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 13 na kumuuwa huko Likoni.

Mshatakiwa huyo atafunguliwa mashataka hayo Januari mwaka ujao baada ya kubainika kuwa jaji anayehusika kufanya kesi za mauwaji yuko likizoni.