Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mshukiwa wa ugaidi Shee Mohamed Kale amepata afuaeni baada ya Mahakama ya Mombasa kumuachilia huru baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka.

Mwendesha mashtaka Eugine Wangila, aliwasilisha ombi mahakamani siku ya Ijumaa mbele ya Hakimu Richard Odenyo, ya kutaka mahakama kumuachilia mshukiwa huyo kwa ukosefu wa ushahidi, baada ya uchunguzi kukamilika.

Mshukiwa huyo amekaa korokoroni kwa siku kumi baada ya kukamatwa kwake.

Shee Mohamed Kale alitiwa mbaroni mnamo Februari 22, 2016 katika eneo la Kaloleni na kuhusishwa na kilipuzi kilichowaua maafisa sita wa polisi tawala katika eneo la Milimani, huko Lamu mnamo Januari 26, 2016.