Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshukiwa wa ugaidi, Mohamed Kombo, atalazimikia kusalia korokoroni kwa siku 30 kusubiri uchunguzi dhidi yake kukamilika.

Hii ni baada ya afisa wa uchunguzi Samuel Ouama kuwasilisha ombi hilo siku ya Jumatano, mbele ya Hakimu Richard Odenyo kutaka kupewa muda zaidi kufanya uchunguzi dhidi ya madai yanayomkabili mshukiwa huyo.

Hakimu Odenyo alikubali ombi hilo na kuagiza mshukiwa kuzuiliwa kwa siku 30 katika Kituo cha polisi cha Makupa.

Kombo anadiwa kuwa kati ya moja wa washukiwa wasita waliokwepa mtego wa polisi katika eneo la Majengo Shikamoo mnamo Januari 4, 2016.

Kombo alitiwa mbaroni Januari 13, 2016, katika eneo la Mikindani, kwa madai ya kuhusika na kundi la al-Shabaab.