Mshukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya Hassan Omari Abdallah atasalia korokoroni kwa siku saba ili kusaidia polisi kukamilisha uchungizi wao.
Hii ni baada ya afisa wa upelelezi Joseph Indeke kuwasilisha ombi mbele ya Hakimu Diana Mochache siku ya Jumatano la kutaka kupewa muda zaidi wa kukamilisha uchunguzi wake.
Hassan alitiwa mbaroni siku ya Jumanne katika eneo la Mtwapa na kuhusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya.
Hakimu Mochache alikubali ombi hilo na kuagiza mshukiwa kuzuiliwa katika Kituo cha polisi cha Reli.