Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamume mmoja alifikishwa mbele ya Mahakama ya Winam, jijini Kisumu, siku ya Jumatatu kujibu shtaka la wizi wa mabavu.

Upande wa mashtaka ulieleza mahakama kuwa mnamo Desemba 9, 2015 mshtakiwa, Peter Otieno, ambaye ni bawabu, aliyeajiriwa na kampuni ya Pride Kings Service, alikuwa amepewa jukumu la kulinda makazi ya Caroline Ogutu mtaani Migosi jijini Kisumu.

Otieno anadaiwa kushirikiana na watu wengine ambao hawakua mahakamani, kuiba mali ya mlalamishi yenye thamani ya shilingi 110,000.

Mshtakiwa alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Caroline Njalali, na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.

Kesi hiyo itasikilizwa mnamo Aprili 18, 2016.