Mwanamke mwenye umri wa miaka 30 alifikishwa mbele ya hakimu mtendaji wa Kisumu siku ya Jumanne kujibu shtaka ya wizi wa runinga, radio na simu.
Agnes Kombewa, mkazi wa Otongolo, alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Harison Adika.
Upande wa mashtaka ulieleza mahakama kuwa mushukiwa, ambaye ni mwendesahaji bodaboda, anadaiwa kuiba bidhaa hizo kutoka kwa nyumba ya Hellen Apuyo, ambaye alikua amembeba kwenye pikipiki yake mnamo Desemba 1, 2015 jijini Kisumu.
Mahakama ilielezwa kuwa mshukiwa alikua nje ya nyumba ya mlalamishi akisubiri malipo yake, anapodaiwa kutekleza wizi huo.
Kiongozi wa mashtaka alisema kuwa mshukiwa aliagizwa na Apuyo kumsubiri kidogo aende msalani kujisaidia, kabla ya kumpa malipo yake.
Apuyo aliporejea kutoka msalani, ndipo alipogundua kuwa bidhaa zake za elektroniki hazikuwa.
Mlalamishi huyo alisema kuwa aliamua kuulizia majirani wake na hapo ndipo alipoelezewa kuwa mhudumu wa pikipiki aliyekuwa amembeba ndiye aliyeonekana na bidhaa hizo.
Apuyo alisema kuwa alienda katika kituo cha polisi ambako aliripoti kisa hicho ba msako dhidi ya mshtakiwa ukaanzishwa mara moja.
Mshtakiwa alikamatwa nyumbani kwake mnamo Disemba 10, ambapo bidhaa hizo zinadaiwa kupatikana sebuleni mwake.
Kombewa aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 20, 000 huku kesi hiyo ikitarajiwa kuendelea Januari 20, 2016.