Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamume mmoja amefikishwa katika mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la wizi wa gurudumu la gari.

Upande wa mashtaka uliambia mahakama siku ya Jumatano kuwa mshtakiwa, Omar Mwazani Zani, anadaiwa kuiba gurudumu pamoja na betri ya gari, zote zikiwa mali yenye thamani ya shilingi 22,000, mnamo Februari 10, 2016, katika eneo la Kona Mpya Likoni.

Mshtakiwa alikanusha madai hayo mbele ya hakimu katika mahakama ya Mombasa Richard Odenyo.

Hakimu Richard Odenyo alimpa mshtakiwa dhamana ya shilingi 30,000.

Kesi hiyo imeratibiwa kusikizwa tarehe Machi 17, 2016.