Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mshukiwa wa wizi alipokea kichapo cha mbwa kutoka kwa wakaazi wa eneo la Kizingo, baada ya kudaiwa kupatikana akijaribu kuiba vipuri vya gari aina la BMW siku ya Jumatano.

Mshukiwa huyo, Khulthum Masjid, alivamiwa na umati wa watu walioudhika na kitendo hicho.

Mshukiwa huyo anadaiwa kuwa na gari nyingine aina ya Voxy, aliyokuwa akitumia kama mahali pa kuweka vipuri hivyo alivyoiba.

Alipovamiwa na umati, mshukiwa huyo alijaribu kubembeleza umati huo usimuue lakini wakaazi hao wakaendelea kumwadhibu.

Masjid aliokolewa na maafisa wa polisi walio wasili katika eneo hilo na kumpelekwa katika kituo cha polisi.